Jinsi ya Kuboresha Lishe Yako "Usile kitu ambacho bibi yako asingeweza kutambua kama chakula. Kuna vitu vingi vinavyo fanana na chakula kwenye supermarkets ambavyo watangulizi wako wasingevitambua kama chakula... epuka vitu hivi." Michael Pollan Lishe Bora ni nini? Inakulinda dhidi ya magonjwa hatari yasiyo ya kuambukiza, kama vile ugonjwa wa moyo, kisukari na saratani. Kula vyakula vyenye kiasi kidogo cha chumvi, sukari na mafuta yatokanayo na wanyama ni muhimu kwa afya yako. Lishe bora hujumuisha mchanganyiko wa vyakula tofauti kama vile: Vyakula vya nafaka (mahindi, ngano, mchele au shayiri) au mizizi yenye wanga (mihogo, viazi, au viazi vitamu) Mbegu jamii ya kunde (maharage, dengu, n.k.) Matunda na mboga za majani Vyakula kutoka kwa wanyama (nyama, samaki, maziwa na mayai) Kufahamu tu ni vyakula gani unapaswa kula haitoshi! Ratiba ya kula na chanzo cha vyakula vina umuhimu mkubwa katika afya yako, katika makala haya tutazungumzia vyakula gani ule, muda gani na kwa...
Stay Informed, Stay Healthy