Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2024

UKWELI KUHUSU P2

p2 ni nini?  " Morning pills" ama " p2"  kama zinavyofahamika na watu wengi mtaani, ni dawa za dharura zinazotumika kuzuia mimba. p2 zina homoni inayoitwa "levenogesterol" ambayo hufanya kazi ya kuzuia mimba kwa njia kuu tatu:  Huzuia yai kutolewa (Ovulation) Huzuia mbegu ya kiume kukutana na yai (Fertilization) Huzuia yai lililotungwa kujishikiza kwenye mji wa uzazi (Implantation)  Dawa hizi ni kwa ajili ya dharura tu, na hufanya kazi ndani ya masaa 72 baada ya kufanya tendo ka ndoa bila kinga, ufanisi wake unaweza kufika hadi asilimia 95 ikiwa zitatumika mapema.  Mara ngapi nitumie p2? Ni salama kutumia p2 mara moja katika mzunguko mmoja wa hedhi , matumizi ya mara nyingi ndani ya mzunguko mmoja wa hedhi yanaweza kusababisha madhara makubwa zaidi ya homoni na mzunguko wa hedhi.  Matumizi ya mara kwa mara yanaweza kusababisha mzunguko wa hedhi usio tabirika, kutokuwepo kwa hedhi kwa muda mrefu, au kutokwa na damu isiyo kawaida (spotting).  p2 zinabeba...