Dawa hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto wako, na tuwe wakweli tu, kuna watu wako kwenye hizi "pharmacy" zetu, hawajali kabisa na pengine hawajui dawa ipi ni salama kwa mtoto ama la!
Hakikisha unasoma karatasi ya maelezo iliyopo ndani ya boksi la dawa kwa uhakiki na ufahamu zaidi. Tutumie msemo wa kimombo unasema "Better safe than sorry"
Haya ni baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa hii:
- Hatari kubwa kwa MOYO
Domperidone inaweza kuathiri mfumo wa umeme wa moyo na kuongeza muda wa QT (QT prolongation). Hii inaweza kusababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (arrythmia), hali ya hatari inayoweza kutishia maisha isipo dhibitiwa haraka.
- Matatizo ya mfumo wa fahamu
Domperidone hufanya kazi kwa kuongeza kasi ya utumbo na kuzuia kemikali fulani kwenye ubongo (dopamine antagonist). Ingawa madhara yake makubwa yanahusiana na moyo, pia inaweza kuathiri mfumo wa fahamu na kusababisha seizures (kifafa), hasa kwa watoto wadogo.
Domperidone haiwezi kuvuka kwa urahisi kizuizi cha damu kwenye ubongo (blood-brain barrier), lakini kwa watoto wachanga au wale walio na mfumo wa neva usioimarika, kuna uwezekano mkubwa wa dawa hii kuathiri ubongo moja kwa moja. Hili linaweza kusababisha:
✅ Misuli kujikaza isivyo kawaida (dystonia)
✅ Mtoto kuwa na mitetemo isiyo ya kawaida (tremors)
✅ Seizures (degedege/kifafa), hasa kwa watoto walio na historia ya kifafa au walio na hatari ya matatizo ya mfumo wa neva
✅ Misuli kujikaza isivyo kawaida (dystonia)
✅ Mtoto kuwa na mitetemo isiyo ya kawaida (tremors)
✅ Seizures (degedege/kifafa), hasa kwa watoto walio na historia ya kifafa au walio na hatari ya matatizo ya mfumo wa neva
- Maumivu ya tumbo na matatizo ya mmeng'enyo
Domperidone huathiri utumbo kwa kuharakisha usafirishaji wa chakula, jambo ambalo linaweza kusababisha kuhara, maumivu ya tumbo, au gesi nyingi kwa baadhi ya watoto.
Comments
Post a Comment