Dawa gani nisitumie kama nina Kisukari? Katika sayansi ya dawa kuna kitu kinaitwa muingiliano (drug interaction), hii inaweza kuwa muingiliano kati ya dawa na dawa, muingiliano kati ya dawa na ugonjwa, au muingiliano kati ya dawa na chakula. Katika makala hii tutaangazia muingiliano wa dawa na ugonjwa wa kisukari pia muingiliano wa baadhi ya dawa na dawa za kisukari, kuna dawa ambazo zinaweza kusababisha sukari ya mwili kupanda, au dawa ambazo zinaweza kuzuia dawa zako za kisukari zisifanye kazi yake vizuri. Kisukari ni nini? Kisukari ni hali ambayo husababisha kiwango cha sukari katika damu kuwa juu isivyo kawaida. Kulingana na sababu zinazoweza kusababisha hali hii, kuna aina mbalimbali za kisukari: Kisukari Aina ya 1 (Type 1 Diabetes) Hii ni hali ambapo mwili hauwezi kuzalisha insulini kabisa. Hii ni kwa sababu seli za kongosho (pancreas) zinashambuliwa na mfumo wa kinga wa mwili na kuharibiwa. Hali hii inaweza kuwa ya kurithi na mara nyingi huanza utotoni au ujana, lakin...
Stay Informed, Stay Healthy