Skip to main content

Posts

DOMPERIDONE SYRUP: HATARI KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 12!

Unapofika duka la dawa kuulizia dawa ya kuzuia kutapika kwa mtoto wako, kuwa makini! Sio kila dawa ya mfumo wa kimiminika (syrup) inafaa kwa mtoto, HAPANA.  Dawa hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto wako, na tuwe wakweli tu, kuna watu wako kwenye hizi "pharmacy" zetu, hawajali kabisa na pengine hawajui dawa ipi ni salama kwa mtoto ama la!  Hakikisha unasoma karatasi ya maelezo iliyopo ndani ya boksi la dawa kwa uhakiki na ufahamu zaidi. Tutumie msemo wa kimombo unasema "Better safe than sorry" Haya ni baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa hii:  Hatari kubwa kwa MOYO Domperidone inaweza kuathiri mfumo wa umeme wa moyo na kuongeza muda wa QT ( QT prolongation ). Hii inaweza kusababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (arrythmia), hali ya hatari inayoweza kutishia maisha isipo dhibitiwa haraka.  Matatizo ya mfumo wa fahamu Domperidone hufanya kazi kwa kuongeza kasi ya utumbo na kuzuia kemikali fulani kwenye ubongo (dopamine antagonist). Ingawa...
Recent posts

Nyama Nyekundu na Hatari Zake!

  Hatari za Afya Zinazohusiana na Ulaji wa Nyama Nyekundu Nyama nyekundu, kama vile nyama ya ng’ombe, mbuzi, na kondoo, ni chanzo kizuri cha protini, madini ya chuma, na zinki. Hata hivyo, ulaji mwingi wa nyama nyekundu umehusishwa na hatari mbalimbali za kiafya.  Makala hii inakufahamisha zaidi kuhusu hatari hizi na jinsi unavyoweza kuboresha lishe yako kwa njia salama. 1. Magonjwa ya Moyo Nyama nyekundu, hasa iliyo na mafuta mengi, inaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo. Mafuta (saturated fat) : Hupandisha kiwango cha lehemu (cholesterol) mwilini, na hivyo kuathiri afya ya moyo. TMAO (Trimethylamine-N-oxide) : Kemikali inayozalishwa tumboni wakati wa kumengenya nyama, ambayo inahusishwa na matatizo ya magonjwa ya moyo.  2. Kansa ya Utumbo Mkubwa (Colon Cancer) Utafiti umeonyesha kuwa ulaji wa nyama nyekundu, hasa iliyosindikwa kama sausage na bacon, unaongeza hatari ya kansa ya utumbo. Nyama zilizochakatwa: Matumizi ya mara kwa mara ya "sausage" na "bacon" ya...

Tunda: Pipi Asilia

Kwa Nini Watoto Wapende Matunda Badala ya Vitamu vya Kiwandani? Watoto wengi hupenda vitu vitamu kama pipi na biskuti, lakini je, unajua jinsi unavyoweza kuwafanya wapende matunda zaidi?  Ni rahisi kuelewa kwa nini vitamu hivi vina radha nzuri na mara nyingi huonekana kuvutia. Lakini je, unajua jinsi vitamu hivi vinavyoweza kuathiri afya ya mtoto wako kwa muda mrefu?  Badala yake, matunda yanaweza kuwa chaguo lako namba moja. "pipi za asili" zenye afya!  Madhara ya Vitamu vya Kiwandani Vitamu vya kiwandani vina changamoto nyingi ambazo hatuwezi kuzipuuza:  Sukari nyingi : Sukari inayoongezwa kwenye pipi na soda inaweza kusababisha kuoza kwa meno , uzito kupita kiasi , na matatizo ya muda mrefu ya kisukari .  Kalori tupu : Vitamu hivi havina virutubisho muhimu, badala yake vinatoa nishati isiyo na faida yoyote mwilini. Hii husababisha watoto kupata nguvu ya muda mfupi ikifuatiwa na uchovu, hali inayoweza kuathiri umakini wao.  Hudhoofisha kinga ya mwili : Su...

UKWELI KUHUSU P2

p2 ni nini?  " Morning pills" ama " p2"  kama zinavyofahamika na watu wengi mtaani, ni dawa za dharura zinazotumika kuzuia mimba. p2 zina homoni inayoitwa "levenogesterol" ambayo hufanya kazi ya kuzuia mimba kwa njia kuu tatu:  Huzuia yai kutolewa (Ovulation) Huzuia mbegu ya kiume kukutana na yai (Fertilization) Huzuia yai lililotungwa kujishikiza kwenye mji wa uzazi (Implantation)  Dawa hizi ni kwa ajili ya dharura tu, na hufanya kazi ndani ya masaa 72 baada ya kufanya tendo ka ndoa bila kinga, ufanisi wake unaweza kufika hadi asilimia 95 ikiwa zitatumika mapema.  Mara ngapi nitumie p2? Ni salama kutumia p2 mara moja katika mzunguko mmoja wa hedhi , matumizi ya mara nyingi ndani ya mzunguko mmoja wa hedhi yanaweza kusababisha madhara makubwa zaidi ya homoni na mzunguko wa hedhi.  Matumizi ya mara kwa mara yanaweza kusababisha mzunguko wa hedhi usio tabirika, kutokuwepo kwa hedhi kwa muda mrefu, au kutokwa na damu isiyo kawaida (spotting).  p2 zinabeba...

DAWA ZA KUEPUKA KAMA UNA KISUKARI

Dawa gani nisitumie kama nina Kisukari? Katika sayansi ya dawa kuna kitu kinaitwa muingiliano (drug interaction), hii inaweza kuwa muingiliano kati ya dawa na dawa, muingiliano kati ya dawa na ugonjwa, au muingiliano kati ya dawa na chakula.  Katika makala hii tutaangazia muingiliano wa dawa na ugonjwa wa kisukari pia muingiliano wa baadhi ya dawa na dawa za kisukari, kuna dawa ambazo zinaweza kusababisha sukari ya mwili kupanda, au dawa ambazo zinaweza kuzuia dawa zako za kisukari zisifanye kazi yake vizuri.  Kisukari ni nini? Kisukari ni hali ambayo husababisha kiwango cha sukari katika damu kuwa juu isivyo kawaida. Kulingana na sababu zinazoweza kusababisha hali hii, kuna aina mbalimbali za kisukari: Kisukari Aina ya 1 (Type 1 Diabetes) Hii ni hali ambapo mwili hauwezi kuzalisha insulini kabisa. Hii ni kwa sababu seli za kongosho (pancreas) zinashambuliwa na mfumo wa kinga wa mwili na kuharibiwa. Hali hii inaweza kuwa ya kurithi na mara nyingi huanza utotoni au ujana, lakin...

SEX IS THE MIND GAME

Understanding the impacts of Stress, Depression and Self-confidence on Sexual Health. Sex is the byproduct of great connection and intimacy, not the replacement for or the source of.  Sexual chemistry and attraction is based on how someone feels more about themselves, rather than their partner. So if you feel you are not as attractive, or you feel you’re not investing yourself in growing, or feeling you’re not becoming more and better, it's unlikely you’re going to want to share your body, mind, emotions and heart with anyone else in the most physical and intimate way which is sex. STRESS Stress is the natural human response that prompts us to address challenges and threats in our lives, a new job for example, or a new relationship, a difficult task you've been given, etc. So a little bit of stress is good, it helps us perform our daily activities.  Too much stress on the other hand, it doesn't do us any good, it can cause physical and mental health problems, one of them is...

Dawa Zinazo Haribika Mapema baada ya Kufunguliwa | Jinsi ya Kuhifadhi kwa Usahihi

 ZIFAHAMU DAWA ZAKO Matumizi sahihi ya dawa si kufuata tu ushauri wa mbili mara tatu! Baadhi ya dawa zina muda maalumu wa kutumika baada ya kuwa zimefunguliwa, hasa dawa zilizoko kwenye mfumo wa maji. Katika makala hii, tutaangazia muda sahihi dawa zinaweza kutumika bila kuleta shida kiafya na jinsi ya kuhifadhi ili kudumisha ufanisi na ubora.  Poda za kuchanganya: Zitumike ndani ya siku 7 tu! Dawa zilizotengenezwa kwa mfumo wa poda, mfano antibiotiki: amoxicillin, ampiclox, n.k. ukisha zichanganya na maji zinaweza kutumika ndani ya siku saba pekee. Baada ya siku saba uwezo wa dawa hizi kufanya kazi hupungua.  Baadhi ya dawa zina maelekezo ya kutunzwa kwenye jokofu (fridge), hivyo soma maelekezo kwenye boksi ama karatasi ya maelezo iliyo ndani ya boksi, ama muulize mtaalamu wa afya jinsi gani ya kuhifadhi dawa zako.  MUHIMU: Hakikisha unafunga vizuri chupa baada ya kila matumizi ili kuepuka kuingiza hewa na vijidudu.  Dawa za maji (syrup): Zitumike ndani ya siku...