Unapofika duka la dawa kuulizia dawa ya kuzuia kutapika kwa mtoto wako, kuwa makini! Sio kila dawa ya mfumo wa kimiminika (syrup) inafaa kwa mtoto, HAPANA. Dawa hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto wako, na tuwe wakweli tu, kuna watu wako kwenye hizi "pharmacy" zetu, hawajali kabisa na pengine hawajui dawa ipi ni salama kwa mtoto ama la! Hakikisha unasoma karatasi ya maelezo iliyopo ndani ya boksi la dawa kwa uhakiki na ufahamu zaidi. Tutumie msemo wa kimombo unasema "Better safe than sorry" Haya ni baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa hii: Hatari kubwa kwa MOYO Domperidone inaweza kuathiri mfumo wa umeme wa moyo na kuongeza muda wa QT ( QT prolongation ). Hii inaweza kusababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (arrythmia), hali ya hatari inayoweza kutishia maisha isipo dhibitiwa haraka. Matatizo ya mfumo wa fahamu Domperidone hufanya kazi kwa kuongeza kasi ya utumbo na kuzuia kemikali fulani kwenye ubongo (dopamine antagonist). Ingawa...
Hatari za Afya Zinazohusiana na Ulaji wa Nyama Nyekundu Nyama nyekundu, kama vile nyama ya ng’ombe, mbuzi, na kondoo, ni chanzo kizuri cha protini, madini ya chuma, na zinki. Hata hivyo, ulaji mwingi wa nyama nyekundu umehusishwa na hatari mbalimbali za kiafya. Makala hii inakufahamisha zaidi kuhusu hatari hizi na jinsi unavyoweza kuboresha lishe yako kwa njia salama. 1. Magonjwa ya Moyo Nyama nyekundu, hasa iliyo na mafuta mengi, inaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo. Mafuta (saturated fat) : Hupandisha kiwango cha lehemu (cholesterol) mwilini, na hivyo kuathiri afya ya moyo. TMAO (Trimethylamine-N-oxide) : Kemikali inayozalishwa tumboni wakati wa kumengenya nyama, ambayo inahusishwa na matatizo ya magonjwa ya moyo. 2. Kansa ya Utumbo Mkubwa (Colon Cancer) Utafiti umeonyesha kuwa ulaji wa nyama nyekundu, hasa iliyosindikwa kama sausage na bacon, unaongeza hatari ya kansa ya utumbo. Nyama zilizochakatwa: Matumizi ya mara kwa mara ya "sausage" na "bacon" ya...